jifunze Neno la Mungu
Neno la MUNGU
Neno la Mungu litakuwa nguzo kuu kwako wewe mtumishi wa Mungu uliyemwamini Yesu kristo. Tunakuletea ufafanuzi wa kina wa Maandiko Matakatifu ili uweze kukua katika imani yako na kumtumikia Mungu kwa ukamilifu na uaminifu ili uishi maisha matakatifu na ya kumpendeza yesu wetu kristo aliyekufa kwa ajili yetu sisi wanadamu.
Kila Jumatano,Ijumaa na jumapili kuna mafundisho ya neno la Mungu ili kukupa msingi imara wa kiroho.
Shuhuda Mbalimbali
Shuhuda mbalimbali zitaendelea kukujenga katika safari hii ya kwenda mbinguni.
Matukio Mbalimbali
matukio mbalimbali kuhusu injili,kusifu na kumwabudu mungu, pamoja na shukurani mbele za mungu.
Injili ni uwezo wa Mungu Uletao wokovu kwa mwandamu.
Semina Mbalimbali E.A.G.T Kongwa
Semina ya Kifedha
Jifunze mbinu za kibiashara na uwekezaji. Usikose nafasi hii ya kujua siri za kifedha na namna ya kustawi sana kama mtumishi wa Mungu katika mambo yote.
Semina hii inalenga kuwapa waumini ujuzi wa kusimamia fedha ipasavyo.
Semina ya Ndoa na Familia
Semina ya ndoa na familia hutolewa kanisani ili kuendelea kumjenga Mkristo katika safari ya ndoa.
Tunajadili mada muhimu kama ushirikiano katika ndoa, ulezi wa Kikristo, na jinsi ya kuwa na familia inayomtukuza Mungu. Karibu na Mungu wa mbinguni atakubariki wewe na familia yako.
Semina ya Neno La Mungu
Semina ya Neno la Mungu hufundishwa kanisani ili kuendelea kumjenga Mkristo katika safari hii ya kwenda mbinguni.
Tunazungumzia mafundisho mbalimbali ya kibiblia ili kuwawezesha waumini uwezo wa kuyatumia maishani mwao kila siku. Karibu na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Maono ya Kanisa
huduma ya Compassion
E.A.G.T Kongwa inaendesha huduma ya compassion inayofanya kazi mbalimbali za kijamii na kiroho:
- Msaada kwa yatima na wazee.
- Ujenzi wa shule na vituo mbalimbali vya elimu kwa vitendo kama vile computer course, cherehani n.k .
Jiunge nasi katika kuwahudumia wengine kwa upendo wa Kristo.
Chuo cha Biblia
chuo cha Biblia kipo Wilayani kongwa.Mwenyekiti wa Bodi akiwa ni Bishop DR. Livingstone Denis.Tunapokea wanafunzi toka ndani na nje ya Tanzania, tunatoa vyeti vya Diploma, na tumeendelea kutoa wahitimu wengi wa shule hiyo yaBiblia.
- Theolojia ya Msingi.
- Uongozi wa Kikristo.
- Mafundisho ya Kibiblia.
Karibu ujiandikishe na uweze kutumika katika kanisa la Mungu.
Mkakati wa Kanisa
Kanisa lina mikakati mbalimbali ikiwemo:
- Kufunga na kuomba kwa bidii.
- Kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
- Kumwabudu Mungu aliyeumba mbingu na ardhi.
- Kuwafundisha waumini neno la Mungu kupitia semina na mikutano mbalimbali.
- Kuhudumia watu wenye mahitaji.
Tunawakaribisha watu wote wajiunge na kanisa la E.A.G.T Kongwa ili tuweze kuujenga ufalme wa Mungu kwa pamoja.
Wasiliana Nasi
Tunawakaribisha kwa maswali, maoni na ushirika wako. Wasiliana nasi kupitia njia zifuatazo: